RAIS MWINYI APOKEA TUZO YA ZANZIBAR YA AFRICA'S BEST CORPORATE RETREAT DESTINATION 2025

Coconut Fm Zanzibar

193 Views 0

ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa taasisi na wadau wa sekta ya utalii kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha Tanzania, ikiwemo Zanzibar, inaendelea kunufaika na tuzo na fursa za kimataifa katika sekta ya utalii.

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 12 Desemba 2025, Ikulu Zanzibar, baada ya Rais Dkt. Mwinyi kupokea Tuzo ya Africa’s Best Corporate Retreat Destination 2025, ambayo Zanzibar imeshinda kwenye Mashindano ya Dunia ya Utalii wa Safari (World Travel Awards 2025) yaliyofanyika nchini Bahrain.

Tuzo hiyo imewasilishwa kwa Rais na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Hamad Hassan Chande. Ushindi huo ni wa kwanza kwa Zanzibar, baada ya kushindana na mataifa manne: Kenya, Afrika Kusini, Morocco na Botswana.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amesema ushindi huo ni heshima kubwa kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, na unadhihirisha kiwango kikubwa cha maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Amesisitiza umuhimu wa kuongeza ubora wa huduma, kuimarisha vivutio vya utalii, na kutumia tuzo hizo kama chachu ya kushindana kimataifa, hasa katika eneo linalokua kwa kasi la utalii wa mikutano na matukio.

Related Videos