Tanzania Yashinda Tuzo Nne kubwa Duniani za Utalii za World Travel Awards.
Tuzo hizi za Utalii za World Travel zimegawanywa katika makundi mbalimbali ambayo ni tuzo za jumla za Dunia, tuzo za washindi wa kila bara na tuzo za washindi wa nchi husika, ambapo kwenye kipengele cha Dunia Tanzania ilipata Tuzo 4 sawa na Afrika ya kusini na kuwa ndio nchi mbili za Afrika zilizoongoza kwa tuzo nyingi kwenye kipengele hicho.
Tanzania ilishinda tuzo za World leading safari Destination (Eneo bora Duniani la Utalii wa Safari), World Leading Baloon Oparator (Muendeshaji Bora wa Utalii wa Baloon Duniani) kwa Serengeti Baloon Safari, World Leading Safari Company 2024 (Kampuni bora ya utalii wa safari) ikichukuliwa na twiga Tours Pamoja na World Leading Exclusive Private Island 2024 (Kisiwa bora binafsi ya utalii Duniani) kikipata kisiwa cha Thanda kilichopo kisiwani Mafia.
#samiaapp
#kaziiendelee
#utalii